Position 18 in the country - 2017 exam

The Best National School In the Country
Position 18 in the country - 2017 exam

The Best Boys School in Nyeri County

The Best National School In the Country
The Best Boys School in Nyeri County

Kiswahili Section

IDARA YA KISWAHILI – TUNALENGA JUU

Walimu wanaofunza Kiswahili ni wafuatao:

Bwana Mugwe G. (mkuu wa idara). Bwana Ndung’u, Bi. Ng’ang’a, Bwana Karuku, Bwana Mukui na Bi Wachira.

Kiswahili ni lugha ambayo wengi katika shule hii tajika wameendelea kuienzi. Wanafunzi wamejifunga kibwebwe ili kuendelea kuyaimarisha matokeo yao ya Kiswahili. Walimu wameipa lugha hii kipaumbele kwa vile lazima wawahamasishe wanafunzi kufanya vyema. Wamejitolea sabili kuwakosoa wanafunzi wanapoenda mrama, kuwaonyesha wanafunzi mbinu tofauti na mwafaka za kuyajibu maswali. Aidha wamesi:-  Sitiza matumizi ya Kiswahili sanifu huku wanafunzi wakizingatia kanuni zake.

Ni kutokana na juhudi hizi ambapo matokeo mema yameendelea kuonyeshwa kutoka 8.2 (K.C.S.E 2012) hadi 9.2(K.C.S.E 2013). Wanafunzi 58 walipata alama A na A- mwaka huu tunapania kuongeza A na A- katika somo hili. Nina uhakika ya kwamba lengo hili litatimia kwa vile wanafunzi wetu wanafanya utafiti katika maktaba na mazoezi ya kina.

Bw. Mugwe G.

MKUU WA IDARA

 LUGHA YA KISWAHILI

Lugha ya Kiswahili ni lugha mojawapo wa masomo ya lazima ya kufundishwa na kutahiniwa baada ya kufika kilele cha ahulw za msingi na shule za upili nchini Kenya. Hali hii ni ithibati tosha ya kutupambazukia na kutusawiria kua lugha hii ina umuhimu mkubwa katika viwango tofauti vikiwemo; mahuluki binafsi, jamaa zake , jamii na zaidi ya yote taifa zima bila kusahau kimataifa. Hadhi zake zimekifanya kitukuke na kusifika si haba. Baadhi ya hadhi zake ni pamoja na: Hadhi ya kitaifa, kumaanisha kuwa asili yake ni humu nchini Kenya: Lugha ya taifa, maana kuwa hutumiwa kudhihirisha utamaduni wa taifa letu huru na kuleta umoja wa jamii tofauti nchini. Aidha kina hadhi ya kuwa lugha rasmi.

 Urasimi huu ulitoka na kuidhinishwa kwa katiba mpya mwaka wa 2010 ambapo sasa lugha rasmi nchini Kenya ni Kiswahili na Kingereza bali si kingereza na Kiswahili. Hali hii imesaidia kwa kiasi ukoloni mamboleo wa kilugha.urasmi huu hukiwezesha kutumiwa katika miktadha aghalabu yote rasmi. Hadhi ya mwisho ni kuwa Kiswahili ni lugha ya kimataifa. Hali hii inamaanisha kuwa lugha hii inasemwa, kufundishwa shule nyingi duniani, kutangazia, kufanyia biashara na kuendesha makongamano mfano wa  umoja wa mataifa ya Africa.

Dhana, fasili, maelezo haya ndiyo yanayotia kuongeza na kuzidisha hamu, ari na nguvu katika idara ya Kiswahili katika shule ya upili ya wavulana ya Kagumo. Shule inaidara ya Kiswahili na wafuatao ni walimu wake.

 Bw. Mugwe G  -  Mkuu wa Idara.

Bw. Karuku S.

Bw. Mukui j.

Bw. Ndung’u W.

Bi. Ng’ang’a R.

Bw P. Kamithi

 Aidha kuna walimu wengine wanaotoa misaada ili kuongeza utendakazi kwa jumla. Mbinu na mikakati anuwai hutumiwa kuwasilisha somo hili. Pia, michango kutoka makomgamano, warsha, majadliano na walimuu wa shule tofauti hufanywa ili kubadilishana mawazo. Mwaka jana tuliweza kupata alama ya wastani ya B za pointi 9 mwaka huu, tunalenga kupata alama ya wastani ya B chanya (B+).

 Uwezekano wa kupata alama ya A hasi au A kamili unawezekana ikiwa mtazamo chanya utakuzwa miongoni mwa wanafunzi. Hi itatokana na walimu na wanafunzi kuwekeza, kutalii na kuwaandaa wanafunzi vikamilifu hosa katika kidato cha kwanza na cha pili. Kwa mtazamo huu, wanafunzi watapata dhana na vipengele vya kimsingi vya kuwawezesha kupambana na vipengele vingine vya juu zaidi. Mtazamo chanya ukikuzwa mapema, wanafunzi wataelewa manufaa yake kwa kufanya bidii na bila shaka alama ya wastani ya A itapatikana na itakuwa ya uhalisia. Langu ni kuwahimiza wanafunzi kuvitalii vipengele vyote vya lugha ya Kiswahili katika karatasi zote kwa utaratibu mzuri bali si kwa pupa. Vipengele hivi ni pamoja na; insha zote, ufahamu, ufupisho, sarufi na matumizi ya lugha, isimujamii, fasihi andishi na fasihi wsimulizi. Aidha nawatakia kila la heri wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mitihani katika viwango vyote vya elimu hasa wanaongojea mtihani wa KCSE. Nawaombea mpate alama ya A ya Kiswahili kwenye karatasi ya matokeo ya mtihani wa 2014. Jinyime wakati huu kwa kufanya bidii na utafurahi baadaye. Kuishi kwingi kuona mengi.

 Bw. Karuku S.

Idara ya Kiswahili

Shule ya upili ya Kagumo.

Quality Assurance

This department is one of the most senior departments in the school. It was created with the aim of promoting academic performance in the school. The department comprises:-

Read More

Location Map

Who's Online

We have 88 guests and no members online

Reach Us

call

Kagumo High School - Nyeri

Phone: 0721639848

Email: kagumohi@gmail.com

 

Join us on FaceBook

Score card

Why we Do well

 1. Organizing Academic clinic 
 2. Extra teaching and supplementary exams 
 3. Recognition of high achievers 
 4. Grouping students 
 5. Setting school, class and individual targets 

Testimonials

They once declared that as much as our future is uncertain it is wise to endeavor in a business that you are proud of. A four year journey through the four blocks of this prestigious institution has granted me a chance to endeavor in what I derive my pride in; knowledge. In all its avenues I have gained it and can proudly declare myself a gentleman of consolidated intellect. Brian Mwangi - School President

 

 

Our Values and Principles

Values and principles

The mission and vision achievements will be guided by the following values and principles

 • Fear of God
 • Justice
 • Discipline
 • Hardwork
 • Respect
 •   Responsibility
 • Self esteem

Religion

Islamic Society

In the name of Allah, the Most Gracious the Most Merciful;

Aslam Alaikum Warahmatullahi Wabarakatu….

 As Kagumo Islam Society Members, we thank the Kagumo fraternity for their support and also grateful to our teachers as they have tolerated our schedule in prayers and also the administration for supporting us.   By: Chairman of Islamic Society – Abdi Qalaq Mohamed.

JoomShaper